Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema sheria ambazo zinahitaji marekebisho madogo zitafanyiwa kazi haraka huku nyingine zitachukua muda kidogo kulingana na muda wa mchakato wa utekelezaji.
Rais Samia amesema hayo leo Oktoba 21,2022 Ikuku Dar es Salaam wakati akipokea ripoti ya kikosi kazi cha Kutaribu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vyua siasa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Aidha miongoni mwa mapendelezo yaliyotolewa na Kikosi Kazi ni kuruhusiwa kufanyika kwa mikutano ya hadhara kwa mujibu wa Katiba na Sheria pamoja na kuzingatia asilimia 40 ya jinsi katika vyombo vya maamuzi vya vyama vya siasa.
Rais Sami ameunga mkono pendekezo la kufanya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa kwani kutumia Sheria na Kanuni za awali zingeendelea kusababisha changamoto na dosari ziloizokuwa zikijitokeza mwanzoni.
Rais Saia pia amevitaka vyama vya siasa kutahmini mienendo ya vyama vyao hasa kuzingatia usawa wa kijinsi, matumizi mazuri ya fedha, utawala bora na kutokomeza ukatili wa kijinsi kwa kuwawezesha wanawake kugombea nafasi muhimu.
Vilevile, Kikosi Kazi hicho kimependekeza utaratibu mpya wa kupata wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, utendaji wa Tume uruhusiwe kuhojiwa kwenye Mahakama ya juu na pia isilamike kufuata amri ya mtu yeyote , idara yoyote ya Serikali chama chochote cha siasa au taasisi yoyote.
Kikosi Kazi hicho chenye wajumbe 24 na kilichowasilisha maeneo 9 ya kufanyiwakazi, kimependekeza matokeo ya Uchaguzi wa rais yahojiwe kwenye Mahakama ya Juu mara itakapoanzishwa.