Rais Samia ateta na Rais Tshisekedi jijini Kinshasa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya kuwasili katika Jiji la Kinshasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya mazungumzo yao katika Jiji la Kinshasa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Jean-Michel Sama Lukonde Kyenge mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa N’Dijili Kinshasa nchini DRC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 42 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 Agosti, 2022 nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa N’Dijili Kinshasa nchini DRC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 42 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 Agosti, 2022 nchini humo. (Picha na Ikulu)