Aliyekuwa mgombea urais wa Kenya, kupitia wa Azimio la Umoja, Raila Odinga Raila, amekataa matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 9, 2022, yaliyotangazwa jana na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya, Wafula Chebukati.

Jana, Chebukati alimtangaza mgombea urais kupitia Kenya Kwanza Dk William Ruto kuwa mshindi kwa kupata kura milioni 7.1 (asilimia 50.49) dhidi ya kura milioni 6.9 (asilimia 48.85) alizopata Odinga.

Wagombea wengine kwenye uchaguzi huo ni George Wajackoyah aliyepata kura 61,969 (asilimia 0. 44) na David Waihiga alipata kura 31,987.

Raila ambae alifika Ukumbini hapo akiambatana na mgombea Mwenza Martha Wangare Karua pamoja wa viongozi wengine amesema hakubaliani na uamuzi wa Tume Huru na Mipaka IEBC kuwa haikuwa sawa na kwamba tume hiyo imekiuka yale ambayo Wakenya wenyewe wamefanya.

“Tumegundua hitilafu ambayo imefanyika katik IEBC ambayo imejaribu kutaka kukiuka yale ambayo wakenya wenyeye walikuwa wamefanya, tumeona yale yaliyokuwa yamefanywa na mwenyekitgi wa tume Waafula chabukati kujaribu kupindua ile uamuzi wa wakenya anafanya hivyo bila kushauriana nawale wenziye ambao wako pale katika tume ya uchaguzi. amesema Raila

Sisi wana Kenya na Wana-Azimiao tunapenda amani, tunapenda umoja wa Kenya, tunapenda kuwaona Wakenya wakiungana kama kitu kimoja.

By Jamhuri