Mwenyekiti wa Tume ya Uvaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya, Wafula Chebukati ametangaza mgombea wa kiti cha urais William Ruto kuwa mteule wa nafasi ya kiti cha uraiswa kupata kura 7,176,141 sawa na asilimia 50.49.

Mgombea huyo ambaye amechuana vikali kati yake na mgombea wa Azimio la Umoja, Raila Odinga ambaye amepata zaidi ya asilimia 48.

Ruto amewashinda wagombea wenzake Raila Odinga, mgombea wa Chama cha Agano, David Waihiga ambaye alitangaza jana kushindwa na Profesa George Wajackoyah wa Chama cha Roots.

By Jamhuri