Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wageni mbalimbali wakati wa Hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Viongozi pamoja na Washiriki wa Mkutano Mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya African Food Prize 2023 kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Pan-Afrika Bean Research Alliance (PABRA) ambaye pia ni Mkuu wa Mradi wa Maharage Dkt. Jean Claude Rubyogo kwa niaba ya Taasisi hiyo yenye Makao Makuu nchini Kenya wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Viongozi pamoja na Washiriki wa Mkutano Mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Septemba, 2023. Katikati ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa African Food Prize akishuhudia
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye hafla ya Chakula cha Jioni kwa ajili ya washiriki wa Mkutano mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Septemba, 2023.
Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye akiwa kwenye hafla ya Chakula cha Jioni Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Septemba, 2023.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Goodluck Jonathan kando ya mkutano Mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Septemba, 2023.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Goodluck Jonathan, Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn, viongozi wengine pamoja na mshindi wa African Food Prize 2023, Mkurugenzi wa Taasisi ya Pan-Afrika Bean Research Alliance (PABRA) ambaye pia ni Mkuu wa Mradi wa Maharage Dkt. Jean Claude Rubyogo (aliyeshika Tuzo) wakati Hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Viongozi pamoja na Washiriki wa Mkutano Mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Septemba, 2023.
Please follow and like us:
Pin Share