Na Daniel Limbe, JamhuriMedia, Chato

Rais Samia Suluhu Hassan amewaarika wafanyabiashara wa nchi wanachama wa Afrika Mashariki (EAC) kutumia bandari ya Nyamirembe Chato mkoani Geita kusafirisha mizigo yao kwa gharama nafuu na kwa haraka zaidi.

Mbali na hilo,Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) imetangaza ahueni ya kutunza mizigo itakayohifadhiwa kwenye bandari hiyo kutoka siku saba za awali hadi siku 30 na kwamba hatua hiyo inalenga kuwavutia wafanyabiashara wengi kusafirisha mizigo kupitia meli badala ya barabara.

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Deusdedith Katwale,

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Marthine Shigela,akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza kwenye eneo la bandari hiyo ametumia fursa hiyo kuwaeleza umuhimu wa bandari ya Nyamirembe katika kukuza uchumi wao,halmashauri,mkoa, taifa na nchi wanachama wa jumuia ya afrika mashariki kwa ujumla.

Hata hivyo amesema kuzinduliwa kwa bandari hiyo,ni maelekezo aliyopewa na rais Samia Suluhu, ambaye anatamani kuona ushirikiano wa kibiashara wa nchi wanachama unaimalika kupitia bandari hiyo huku akiwataka wafanyabiashara wakubwa wa ndani ya nchi kuchangamkia fursa za kibiashara kwa lengo la kukuza uchumi wao na taifa.

Mkuu wa idara ya utekelezaji wa bandari (TPA) ziwa viktoria, Fransisco Mwanga.

“Maelekezo haya nimetumwa na rais Samia niwaeleze wananchi mtambue rasmi bandari hii inaanza kazi baada ya kuwa ujenzi wake umakamilika kwa aslimia 100…ambapo ghati hili lina uwezo wa kupokea meli saba kwa wakati mmoja” amesema.

Kadhalika ameelekeza meli kubwa zinazotoa huduma ndani ya ziwa kufanya safari zake kupitia bandari ya Nyamirembe ili kuinua uchumi wa mkoa wa Geita huku akiwataka wananchi kuendelea kuzalisha mazao kwa wingi ili kujipatia kipato cha kutosha kutokana na fursa za kibiashara ndani na nje ya nchi.

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Deusdedith Katwale, mbali na kumshukuru rais Samia kwa kuruhusu bandari hiyo kuanza kazi, amesema kurejeshwa kwa huduma ya hiyo kutasaidia sana kuinua uchumi wa wananchi wa ukanda wa Chato, Biharamulo, Ngara,Muleba pamoja na nchi jirani za Rwanda, Burundi na Uganda.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Marthine Shigela

Awali Mkuu wa idara ya utekelezaji wa bandari (TPA) ziwa viktoria, Fransisco Mwanga,amesema eneo la bandari hiyo lilipimwa tangu mwaka 1954 likiwa na ukubwa wa ekari 126 ambapo kwa kipindi cha miaka ya 1880 hadi mwaka 1990 bandari hiyo ilikuwa ikihudumia meli ya Mv Serengeti, Mv Liemba, Mv Ukerewe na Mv Klarias kwa kusafirisha abiria na mizigo katika maeneo ya ukanda wa ziwa viktoria.

Kwamba bandari hiyo ilisimama kufanya kazi tangu mwaka 2002, ambapo mnamo mwaka 2017/18 serikali kupitia TPA ilitenga fedha kiasi cha bilioni 4.1 kwaajili ya ukarabati na ujenzi mkubwa wa bandari hiyo na kwamba mkandarasi alianza kazi mwaka 2018 na kukamilisha mwaka 2019 lakini tangu kukamilika kwake bado haikuwa ikifanya kazi.

Kutokana na hali hiyo,Mwanga amesema jitihada za kuongea na wenye meli zinafanyika ili kurejesha safari za bandari ya Nyamirembe ikiwa ni pamoja na kuondoa gharama za kutunza mizigo kutoka siku saba za awali hadi siku 30.

Diwani wa kata ya Nyamirembe,Bashir Manampa,akielezea umuhimu wa Bandari ya nyamirembe kwa jamii.
             

By Jamhuri