Na Mwandishi Wetu JAMHURI MEDIA, Lusaka Zambia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais wa Jamhuri ya Zambia Hakainde Hichilema kuweka maua katika mnara wa Mashujaa uliopo viwanja vya uhuru kama ishara ya kuadhimisha miaka 59 ya uhuru wa taifa hilo.

Pia Rais Samia ameweka shada la maua katika kaburi la Muasisi wa taifa hilo Hayati Kenneth David Kaunda leo Oktoba 24, 2023 Lusaka Zambia.

Taifa la zambia linaadhimisha miaka 59 tangu lijipatie uhuru kutoka mikononi mwa Uingereza mwaka 1964.

Akiwa katika ziara ya siku tatu nchini humo kuanzia Oktoba 23 hadi 25, 2023 Rais Samia ndiye mgeni rasmi katika sherehe hizo.