Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wafanyakazi wa Azam Media mara baada ya kufungua Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited Ndugu Tido Mhando wakati alipotembelea Studio za matangazo za Azam TV zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria ufunguzi wa Mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media kwenye hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Ofisi hizo zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya King’amuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Azam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo kwa Niaba ya Kampuni ya Azam Media Mama Violet Maro Mwanamke wa kwanza Mwandamizi katika fani ya Habari nchini wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023
 
Wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Minara ya kurushia matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) iliyofanyika katika Ofisi za Azam Media, Tabata Jijini Dar es Salaam.
 
 

By Jamhuri