Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mke wa aliyekuwa Mfalme wa Qatar Sheikh Hamad Bin Khalifa Al- Thani, Sheikha Moza Bint Nasser Al-Missned wakati alipomtembelea Jijini Doha nchini Qatar tarehe 03 Oktoba, 2023. Mazungumzo yao yalilenga zaidi masuala ya Elimu na jitihada za pamoja za kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokatisha masomo kwa sababu mbalimbali. Sheikha Moza pia ni Mwenyekiti wa Wakfu wa Qatar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Kikao na ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya Power Holding kuhusu maeneo mbalimbali ya Uwekezaji nchini Tanzania. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Kampuni hiyo inayojihusisha na masuala kadhaa ikiwemo Ujenzi, Kilimo na Utalii, Doha nchini Qatar tarehe 03 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Kikao na ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya Power Holding inayojihusisha na masuala kadhaa ikiwemo Ujenzi, Kilimo na Utalii kuhusu maeneo mbalimbali ya Uwekezaji nchini Tanzania. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo Doha nchini Qatar tarehe 03 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia mawasilisho yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Power Holding kuhusu Uwekezaji wanaoufanya katika maeneo mbalimbali Duniani, Doha nchini Qatar tarehe 03 Oktoba, 2023.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia mawasilisho yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Power Holding kuhusu Uwekezaji wanaoufanya katika maeneo mbalimbali Duniani, Doha nchini Qatar tarehe 03 Oktoba, 2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri akizungumza kuhusu fursa mbalimbali za Uwekezaji zilizopo nchini Tanzania kwenye kikao pamoja na viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Power Holding kilichofanyika Doha nchini Qatar tarehe 03 Oktoba, 2023.