Hatimaye kilio cha wanasiasa cha muda mrefu kimepata ufumbuzi baada ya Serikali kuruhusu kuanza kwa mikutano ya hadhara ambayo itazingatia sheria za nchi.

Akizungumza na viongozi wa vyama 19 vya siasa leo Januari 3,2023, Rais Samia amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha mahudhurio ya viongozi wa vyama vya siasa kutoka Tanzania Bara na Visiwani kwani hayo ndiyo aliyokuwa akitaka tangu awali.

Rais Samia amesema kuwa kuna mambo mengi ambayo awali walizungumza na viongozi wa vyama siasa hivyo bado yanaendelea kufanyiwa kazi na maengine yamefanyiwa kazi.

“Kuna mambo yalizungumzwa na kutakiwa kufanyiwa maamuzi.Busara zimenituma kwamba kuna haja ya kufanya taifa kuwa kitu kimoja.

‘Wote tuzungumze lugha moja’ ili taifa liwe moja ni lazima kuwe na maridhiano sisi vyama vya siasa tunaowakilisha vyama siasa hivyo nimeona ni vyema kwanza kuzungumza na vyama vya siasa,” amesema.

Rais Samia amekipongeza kikosi kazi kwa kazi nzuri waliyofanya na hivyo mapendekezo waliyotoa yatafanyiwa kazi ili kujenga taifa moja.

“Mbali ya kuwepo kwa vuta ni kuvute na kufanyika kwa mikutano si chini ya mara sita ama saba na CHADEMA lakini sasa tunakwenda boti mpja, ndio faida ya kukaa meza moja, kwenye mazungumzo amani haikoseni na ndio maana vyoma vyote 19 vipo hapa,” amesema.

By Jamhuri