Watu sita wa familia moja akiwemo baba, anayejulikana kwa jina la Khumbulani Togara, mama na watoto wao wanne, akiwemo kichanga, wanaripotiwa kufariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea siku ya Boxing Day, Desemba 26, 2022.

Ajali hiyo iliyozua gumzo kubwa na taharuki imetokea nchini Afrika Kusini katika eneo la Musina, wakati familia hiyo ikirejea nyumbani kwao, Zimbabwe baada ya kula Krismasi nchini Afrika Kusini.

Video iliyonaswa na kamera za CCTV, imeonyesha tukio hilo ambapo familia hiyo ikiwa ndani ya gari aina ya Mitsubishi ‘double cabin’, ilivaana uso kwa uso na lori lililokuwa kwenye spidi kubwa na kusababisha maafa hayo.

Picha ya pamoja ya wanafamilia walofariki katika ajali enzi za uhai wao

Ajali hiyo imetokea katika Barabara ya N1 kati ya Miji ya Baobab Tollgate na Musina. Inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo, ni uchovu na mwendokasi.

Taarifa hiyo iliripotiwa pia na Ubalozi wa Zimbabwe nchini Afrika Kusini kupitia kwa Balozi Melody Chaurura