Na Wilson Malima, Lusaka Zambia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan tayarì amewasili Ĺusaka Zambia kwa ajili ya ziara ya siku tatu Oktoba 23 hadi 25, 2023.

Rais Samia amewasili na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Hakainde Hichilema katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Keneth Kaunda leo Oktoba 22, 2023.

Katika ziara hii Rais Samia anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuazimisha miaka 59 ya uhuru wa taifa hilo zitakazo fanyika Oktoba 24, 2023 ambapo amepewa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.

Pamoja na mambo mengine, Rais Samia amepewa heshima kubwa kuhutubia bunge la Jamhuri ya Zambia akiwa ni Rais wa Kwanza mwanamke kutoka Tanzania kufanya hivyo, pia anakuwa miongoni mwa watu mashuhuri wanne kuhutubia bunge hilo tangu mwaka 2012

Vilevile Dkt.Samia atapata wasaa wa kuzungumza na wafanyabiashara pamoja na wawekezaji katika kongamano la Biashara kati ya wafanya biashara wa Tanzania na Zambia ambapo pia atakuwa mgeni Rasmi kwenye kongamano hilo.

Hii inakuwa ni ziara ya kwanza ya kitaifa tangu Rais Samia alipohidhuria Sherehe za kuapishwa kwa Rais Hichilema mwaka 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa na mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakifurahia vikundi mbalimbali vya burudani mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.

By Jamhuri