Rais Samia akiwa ziarani mkoani Manyara kwa siku ya pili leo ametembelea na kukagua mirandi mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wa mkoa huo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel wakati akimsikiliza Mganga Mfawidhi wa Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt. Catherine Magali aliyekuwa akielezea maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali hiyo Babati mkoani humo
 leo 23 Novemba, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali Wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara iliyopo Babati katika ziara yake ya siku mbili Mkoani humo tarehe 23 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa akisikiliza maelezo ya Ujenzi wa Ofisi za Chama hicho cha Mapinduzi, Babati Mkoani Manyara tarehe 23 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa akiwasalimia Wananchi mara baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi hizo za Chama Babati Mkoani Manyara tarehe 23 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine wa Chama mara baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi hizo za Chama Babati Mkoani Manyara tarehe 23 Novemba, 2022