Rais Samia:Nawapongeza wanangu Simba Queens kutwaa ubingwa CECAFA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Simba Queens kwa kutwaa taji la Klabu ya Wanawake Afrika Mashariki na Kati jana.

“Nawapongeza wanangu Simba Queens SC kwa ubingwa wa Afrika Mashariki wa CECAFA 2022 kwa Wanawake (SAMIA CUP).

“Mmejenga heshima kwa soka la Tanzania na nchi kwa ujumla. Nawatakia kheri katika Ligi ya Mabingwa Afrika (2022 CAF Women’s Champions League ) itakayofanyika nchini Morocco,” amesema Rais Samia kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Simba ilitwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya She Corporate ya Uganda jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Na sasa Simba Queens imejikatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika ya Wanawake Oktoba mwaka huu nchini Morocco