Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tine Tonnes Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 24 Aprili, 2024.

Pamoja na mambo mengine, Balozi wa Norway amemshukuru Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ziara aliyoifanya hivi karibuni nchini humo ambapo amesisitiza kuwa imeongeza chachu ya mashirikiano ya kidiplomasia sambamba na kukuza jitihada za uwekezaji kwenye maeneo ya kilimo, nishati mbadala, elimu na jitihada za kusaidia miradi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi na athari zake.

Kwa upande mwingine, Dkt Tulia ameishukuru Serikali ya Norway kwa kuendeleza mashirikiano mazuri na Tanzania hususani juu ya miradi wanayoendelea kufadhili nchini. 

By Jamhuri