Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki ni mzima wa afya, imesema taasisi yake.
Imesema hivyo baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii siku ya Jumatano ikizungumzia afya ya rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini na madai kuwa amefariki.
“Tunakanusha taarifa hizo na kuuhakikishia umma kuwa Rais Mbeki ana afya njema,” taarifa ya taasisi hiyo ilisema.
“Tunatoa angalizo kwa watu kuwa makini katika kujihusisha na taarifa za mtandaoni haswa katika kipindi ambacho taarifa za uongo zinaweza kusambaa kwa kasi .”
Hii sio mara ya kwanza kwa bwana Mbeki kulengwa na taarifa ghushi.
Mwaka 2021, wakati wa janga la Uviko 19, baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii walitoa taarifa za uongo kuwa amefariki.
Bwana Mbeki alikuwa rais baada ya Rais Nelson Mandela kuondoka madarakani.
Alihudumu mwaka 1999 mpaka 2008