Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo Septemba 21, 2023 amefanya ziara ya kukagua ufanisi wa uzalishaji wa maji Wilaya ya Ubungo na Kinondoni jukumu ambalo linatekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya maji safi na maji taka ambapo pesa nyingi zinatumika, na upendo mkubwa alionao kwa wananchi na dhamira yake ya kumtua ndoo mama kichwani.

Aidha ameipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa Utekelezaji mzuri wa majukumu yao ambapo kwa sasa DAWASA inauwezo wa kuzalisha Lita milioni 590 kwa siku ikiwa mahitaji halisi ni Lita milioni 540 ” uzalishaji ni hatua moja kubwa na Usambazaji ni hatua nyingi niwapongeze sana” Alisema RC Chalamila

Vilevile Chalamila baada kutembelea miradi ya maji Wazo Wilaya ya Kinondoni na Tegeta A Ubungo amekagua pia mradi wa Uchakataji maji Mbezi Beach ambao utagharimu zaidi ya Dola milioni 63, amesema katika Mkoa huo maji taka ni moja kitu kinachosumbua sana hivyo mradi huo ni mwarobaini wa Changamoto hiyo, amewataka wakandarasi kufanya Kazi hiyo kwa weledi kukamilisha kwa wakati na kwa Ubora na kuzingatia thamani ya pesa pia ametoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano katika Kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo.

Sambamba na hilo Mhe Chalamila ametoa Onyo kwa wadokozi wa vifaa vya Utekelezaji wa mradi huo yayote atakayebainika hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake, hata hivyo amewataka wananchi kuwa mabalozi wazuri katika kutunza vyanzo vya maji na akiwa eneo la shule ya msingi mivumoni kujioenea Usambazaji wa Maji amewataka walimu kutoa elimu maalum ya kulinda vyanzo vya maji kwa wanafunzi ili kuwekeza kwenye kizazi hiki cha leo na cha kesho

Kwa Upande wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Ndg Kiula M. Kingu amemuahidi Mkuu wa Mkoa kuendelea kuboresha pale panapohitaji maboresho kwa masilahi mapana ya watu wengi hususani katika utoaji wa huduma ya maji safi vile vile amesema kukamilika kwa mradi wa kudhibiti maji taka Mbezi Beach kutaleta faida kubwa ikiwemo Mbolea, Umeme (Biogas) maji na kuondoka kana kwa kiasi kikubwa na magonjwa ya milipuko hivyo ametoa rai kwa jamii ambayo mradi unapita kutoa ushirikiano.

Mwisho Mhe Mkuu wa Mkoa katika ziara hiyo aliambatana na Kamati ya usalama ya Mkoa, Viongozi wa Chama ngazi ya Mkoa na wataalam kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira DAWASA wakiongozwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Ndg Kiula M Kingu.

By Jamhuri