Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa pongezi hizo katika sherehe za miaka 25 ya mafanikio ya Kampuni hiyo toka kuanzishwa kwake, hafla iliyofanyika Desemba 16,2023 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Ilala jijini Dar es Salaam.

Akiongea na Watumishi pamoja na wageni waalikwa katika hafla hiyo alipongeza Bodi na menejimenti ya DERM GROUP chini ya uongozi mahiri wa Ridhuan Mringo ambapo amesema kampuni hiyo licha ya kutoa huduma nzuri za kihandisi katika nyanja mbalimbali imetoa fursa kubwa ya ajira kwa watanzania ” Naipongeza DERM GROUP kwa uwekezaji mkubwa katika Human capital kwa kuwa ndio msingi wa kusonga mbele” Alisema Chalamila

Aidha RC Chalamila alisema siku zote katika mafanikio lazima ukutane na Changamoto Success never exists without loosing hivyo kampuni ya DERM GROUP hadi kufikia hapa na leo inasherekea miaka 25 ya mafanikio yako mapito mengi imepitia. “Nipongeze sana kwa kuwa visionary” Alisema RC Chalamila

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya DERM GROUP Mhandisi Ridhuan Mringo alisema Historia imeandikwa kupitia kampuni hiyo ambayo inafanya Shughuli mbalimbali za kihandisi hapa nchini kama vile Real estate, ujenzi wa majengo marefu, Utengezaji wa vifaa vya Umeme na nguzo za Zege ambazo kwa sasa hutumiwa na shirika la Umeme Tanzania(TANESCO)

Please follow and like us:
Pin Share