Na Mwamvua Mwinyi, JammhuriMedia, Mafia

Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Mafia kwa kufanikiwa kuongeza vyanzo vya mapato na kupata hati safi.

Kunenge ameyasema hayo katika kikao cha kujadili hoja za CAG kilichofanyika wilayani Mafia mkoa wa Pwani.

Amesema ,kama kuna vitu ambavyo Mhe.Rais anavisisitiza na kuvitekeleza, halmashauri nyingine zijifunze kuongeza vyanzo vya mapato, vyanzo vipya na kuwa na sheria mpya .

Kunenge ameitaka , halmashauri hiyo ya Mafia kuendelea kubuni na kuwa na vyanzo ambavyo vitaendelea kuongeza ukusanyaji wa mapato ili kuibadilisha Mafia.