📌Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde, kufungua rasmi maadhimisho leo

📌REA kuonesha mchango wa nishati katika kukuza kilimo na uzalishaji wa chakula

📌Wananchi na wadau wakaribishwa kupata elimu kuhusu miradi na fursa za nishati vijijini

📍Viwanja vya Usagara, Tanga

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unawakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kutembelea banda lake katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Usagara, Tanga Mjini, kuanzia Oktoba 10 hadi 16, 2026.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi leo, Oktoba 12, 2026, na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde, yakiongozwa na kaulimbiu “Ubunifu wa Leo, Lishe Bora ya Kesho: Kuelekea Dira 2050.”

Ushiriki wa REA unalenga kuonesha mchango wa nishati katika kuimarisha shughuli za kilimo, uzalishaji, uchakataji na uhifadhi wa mazao, kuongeza tija na kuchochea maendeleo ya kiuchumi vijijini.

Katika banda la REA, wananchi watapata fursa ya kuzungumza na wataalamu wa Wakala, kupata elimu kuhusu miradi ya umeme vijijini, nishati jadidifu, nishati safi ya kupikia na matumizi ya nishati katika shughuli za uzalishaji na biashara.

REA inawakaribisha wakulima, wafanyabiashara, wananchi na wadau wote kutembelea banda lake katika Viwanja vya Usagara, Tanga Mjini, kujifunza na kufahamu fursa za nishati zinazoweza kuongeza tija, kukuza uchumi na kuboresha maisha.