Serengeti girls waendelea kujifua kuikabili Ufaransa

Timu ya Taifa ya Wasichana chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) imeendelea na mazoezi Katika Uwanja wa Utorda Goa India.

Serengeti Girls ilianza na mazoezi ya asubuhi katika fukwe zilizopo eneo la Utorda na baadae katika uwanja wa eneo hilo.

Mazoezi hayo ni katika maandalizi ya Mechi dhidi ya Ufaransa itakayochezwa Oktoba 15 majira ya Saa 4:30 jioni saa za nchini India Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru jijini Goa India.

Katika mazoezi hayo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo Bw. Ally Mayay ameendelea kuwapa hamasa wachezaji hao kuwa uwezo wanao wakupambana na kuwakilisha vyema Taifa.