Waziri Mku Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kumkumbuka Augustino Lyatonga Mrema kutokana na mchango wake mkubwa wa kuendeleza mahusiano na vyama vya siasa.

“Mheshimiwa Mrema atakumbukwa kama kiongozi mkuu wa Chama cha TLP kwa muda mrefu sana. Na akiwa katika siasa, aliisaidia Serikali kupata mwelekeo mzuri wa vyama vya siasa,” amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, baada ya ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema, iliyofanyika katika Kanisa la Roman Catholic Salasala, jijini Dar es Salaam, Agosti 24 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Agosti 24, 2022) wakati akizungumza na mamia ya waombolezaji kwenye ibada ya kumuaga marehemu Mrema katika Parokia ya Mt. Augustino Kilimahewa, Salasala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Wafiwa na Viongozi wa Siasa wakiwa katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema, iliyofanyika katika Kanisa la Roman Catholic Salasala, jijini Dar es Salaam, Agosti 24 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Amesema salamu za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ziliwasilishwa asubuhi na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohudhuria ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema, iliyofanyika katika Kanisa la Roman Catholic Salasala, jijini Dar es Salaam, Agosti 24 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Please follow and like us:
Pin Share