Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar ea Salaam

SERIKALI imesema teknolojia na ubunifu ni muhimu katika kuchagiza maendeleo katika Taifa.

Pia imesema itahakikisha inakuza sayansi, teknolojia na ubunifu nchini , kwalengo la kuchagiza maendeleo na kusaidia kufanyika kwa tafiti zinazojibu changamoto za Watanzania.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam mapema leo Mei 20,2024 na Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya elimu sayansi na Teknolojia Profesa Ladslaus Mnyone kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Profesa Carolyne Nombo katika mdahalo maalum baina ya wahariri, waandishi wa habari na wadau wa ubunifu, uliyoandaliwa na Tume ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (COSTECH) chini ya programu ya ufunguo

Katibu Mkuu huyo amesema katika kuhakikisha sekta ya teknolojia na ubunifu inakua,serikali nimekamilisha mkakati wa teknolojia ya TEHAMA

Kwa upande wake Mkurugenzi wa COSTECH Dk.Amos Nungu, alisema wiki ya bunifu inatarajiwa kuzinduliwa kesho katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere (JNICC), huku kilele chake kikitarajiwa kufanyika mkoani Tanga.

Amesema wiki hiyo ya ubunifu itaenda sanjari na maadhimisho ya miaka 10 ya toka kuanzishwa kwakwake, ambayo Kwa mwaka huu imebebwa na kauli mbiu “Ubunifu kwa maendeleo jumuishi ya rasilimali watu”.

“Katika kuelekea wiki ya ubunifu COSTECH na wadau wa maendeleo tunajivunia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwepo wa uelewa wa pamoja ulioleta matokeo chanya,”amesema Dkt Nungu

Aidha aliongeza kuwa, wiki ya bunifu imeweza kutoa fursa na kuongeza uelewa kwa vijana wengi na baadhi yao wamepata fursa ya kuonekana na kujulikana zaidi.

Naye Meneja Progaramu wa Umoja wa Ulaya Janeth Martoo amesema , ubunifu unahitajika zaidi kwasababu unasaidia katika kukuza ustawi wa uchumi wa taifa.

Amesema licha ya chagamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia chi bado anaamini sekta ya ubunifu ikipewa kipaumbele itaongeza nguvu katika kukuza uchumi.

Naye Meneja Progaramu kutoka funguo, Joseph Manirakiza amesema
katika wiki ya uvumbuzi wanafurahia nguvu ya mageuzi ya juhudi shirikishi katika kuendeleza teknolojia na uvumbuzi.

“Tukio hili linatoa jukwaa kwa wiki ijayo ya kitaifa ya ujuzi wa elimu na uvumbuzi inayoangazia makutano muhimu ya nyanja hizi.

By Jamhuri