Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Tabora

YAPI Merkezi, kampuni ya Uturuki iliyopewa kandarasi na Shirika la Reli Tanzania (TRC) imeanza kujenga awamu nne ya kipande cha reli ya kisasa (SGR) cha Tabora-Isaka kwa kufanya uzinduzi mkubwa ulioshuhudiwa na wageni waalikwa akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Isdor Mpango.

Msingi wa awamu ya nne kutoka Tabora mpaka Isaka unakuja baada ya awamu ya kwanza, pili na tatu ya reli ya Dar es Salaam – Mwanza. Reli hii itakuwa ndefu zaidi kujenga na kampuni jkandarasi ya Uturuki na haraka zaidi ndani ya Afrika Mashariki.

Naibu Meneja mkuu wa kampuni ya Uturuki, Yapi Merkezi, inayojenga reli ya kisasa SGR ndugu Hakan Alkan akitoa maelezo kwa Makamu wa Raisi  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Philip Isdor Mpango kuhusu maendeleo ya mradi wa SGR, katika uzinduzi wa ujenzi wa reli ya SGR LOT 4 kati ya Tabora na Isaka, uliofanyika leo mjini Isaka, mkoani Shinyanga. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Shinyanga Ndugu Mabala Mlolwa na Mkurugenzi wa shirika la reli Tanzania (TRC) Ndugu Masanja Kadogosa.

TRC imeiambia Yapi Merkezi kuweka mipango ya kukamilisha mradi wa kujenga reli ndani ya miezi 42 kutoka Januari 2023.

Miundombinu muhimu inataajiwa kuwekwa wakati wa utekelezaji mradi. Yapi Merkezi imechukua jukumu la kujenga vituo vitatu katikati ya miji ya Tabora na Isaka, kituo cha marekebisho, eneo la mizigo, jengo la utawala, taasisi ya reli, reli yenye urefu wa Kilomita 165, mifumo ya alama za mawasiliano na umeme.

Makamu wa Rais Dkt.Mpango, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, Hakan Alkan na Erhan Cengiz, Makamu Wakurugeni wa Yapi Merkezi Construction, walihudhuria uzinduzi wa ujenzi uliofanyika mjini Isaka Januari, 18, 2023.

Katika hotuba yake Makamu wa Rais amesema, “ Mradi huu wa SGR ni muhimu katika mkakati wa maendeleo ya Tanzania. Zaidi ya fursa 20,000 za ajira zimetengenezwa na jumla ya shillingi trilioni 1.9 za Kitanzania zimekwenda kwa wakandarasi wadogo, ambao wamelipa kodi zinazo kuza pato la taifa”.

Makamu wa Rais aliendelea kwa kupongeza TRC kwa juhudi zao za kuongeza thamani ya pesa kwa wakandarasi wakubwa na wadogo.
“Nina wasihi wakandarasi kufanya kazi kwa uadilifu na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati” amesema.

Naye Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa, alipongeza TRC kwa ushirikiano na mwongozo inaouonyesha katika mradi wa SGR na kuuhakikishia umma kwamba serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasan imedhamiria kuwekeza katika miundombinu ya usafiri ili kuimarisha mifumo ya usafiri inayokwenda kukuza uchumi wa taifa.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Philip Isdor Mpango akimshukuru Naibu Meneja mkuu wa Kampuni ya Uturuki Yapi Merkezi, inayojenga reli ya kisasa SGR, ndugu Hakan Alkan baada ya Makamu wa Rais kukabidhiwa Zawadi na kampuni ya ujenzi ya Reli ya SGR Yapi Merkezi, katika uzinduzi wa ujenzi wa reli ya SGR LOT 4 kati ya Tabora na Isaka, uliofanyika leo mjini Isaka, mkoani Shinyanga. Wengine pichani wakishuhudia ni Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Mh Dk.Mehment Gulluoglu.

Waziri amesema kuwa takribani asilimia 14 ya pato la taifa imeongezeka kutoka na shughuli za usafirishahi bidhaa, huduma na watu.

Yapi Merkezi imetekeleza kwa umahiri miradi yake ya nyuma iliyofanyika nchi mbalimbali duniani na awamu ya nne ni matokeo ya ukamilishaji mzuri wa awamu mbili za kwanza za mradi wa SGR Tanzania.

Kampuni hiyo imefanikisha kikamilifu shughuli zote awamu ya tatu mwezi Desemba 2021 kutokana na mafanikio ya awamu mbili za mwanzo wa mradi.

Akiongea katika halfa ya uzinduzi wa ujenzi wa awamu ya nne yenye urefu wa takribani km 165, Hana Alkan, Naibu Meneja Mkuu wa Construction, alisema “Leo, tunafuraha kuongeza mradi mmoja mwingine tuliofanikisha kuufanya barani Afrika.

“Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania umetuzawadia awamu ya tatu na ya nne ya reli hii ya muhimu kutokana na uadilifu wetu na ubora wa kazi tuliouonyesha katika vipande vya reli viwili vya kwanza, Dar es Salaam-Mwanza chenye urefy wa km 722 kutoka Dar es Salaam mpaka Makutupora, ambacho ni kipande kirefu zaidi cha reli, kuwahi kujenga na kampuni ya Kituruki barani Afrika na chenye mwendo mkali zaidi Afrika Mashariki,” amesema.

Pia Mkurugenzi wa TRC Kadogosa alisema “ SGR itapunguza muda uliokuwa ukipotea kusafirisha bidhaa, huduma na watu, jambo litakalo punguza gharama za usafirishaji bidhaa na huduma pia. Kwa mfano, itachukua takribani masaa 8 kusafiri kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza. Vilevile mradi utafaidisha wakazi wa maeneo ya miji ambapo mradi unafanyika.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Philip Isdor Mpango akiwa kwa picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Uturuki ya Yapi Merkezi, inayojenga reli ya kisasa SGR, waliosimama mstari wa nyuma kwenye sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa reli ya SGR LOT 4 kati ya Tabora na Isaka, uliofanyika mapema leo mjini Isaka, mkoani Shinyanga. Wengine kushoto kwa Makamu wa Raisi ni waziri wa ujenzi na uchukuzi Prof Makame Mbarawa

By Jamhuri