Serikali yaiwezesha MSD kusambaza vifaa tiba, dawa Simiyu Simiyu

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Simiyu

BOHARI ya Dawa (MSD), Kanda ya Mwanza kupitia Serikali imeendelea na usambazaji wa bidhaa za afya katika Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Itilima, licha ya changamoto zinazosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo na nchini kwa ujumla.

Hatua hiyo ni juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suhulu Hasssan, kuhakikisha wananchi wanapata dawa na vifaa tiba kwa wakati bila kujali eneo wanaloishi lina vikwazo vya aina gani vya kimiundombinu.

Kama inavyoonekana pichani, magari yenye vifaa tiba na dawa ya MSD yakiwa yamenasa kwenye barabara mbovu, huku juhudi za kuwananusua zikiendelea ili yaweze kuendelea na safai.

Changamoto za aina hiyo na zaidi ya hizo hata zinazohatarisha maisha ya wafanyakazi wa MSD, imekuwa ni sehemu ya maisha ya kawaida kwa wafanyakazi wa Bohari hiyo, lengo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wanapata vifaa tiba na dawa kwa wakati ili kunusuru afya zao.