Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Arusha

Wizara ya Ardhi na OR-Tamisemi zimesaini mkataba wa makubaliano wa uendelezaji na utekelezaji wa mpango wa matumizi ya shamba lenye ukubwa wa ekari 6176.5 lililopo katika wilaya za Arusha na Arumeru mkoani Arusha.

Utiaji sahihi makubaliano ya shamba la Shambarai Burka na Bwawani ambalo awali lilimilikiwa na Tanzania Plantation Limited umefanyika leo tarehe 28, Agosti Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga pamoja na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Wilson Charles na kushuhudiwa na Wakurugenzi wa Halmshauri za Arusha na Arumeru.

Akiongea kabla ya zoezi la utiaji sahihi wa makubaliano ya mpango wa utekelezaji na mgawanyo wa shamba hilo Katibu Mkuu Sanga amesema shamba hilo lilikuwa na mgogoro kati ya Wizara ya Ardhi na kampuni ya Tanzania Plantations na makubaliano haya yanafanyika baada ya mahakama kuridhia ombi la Wizara ya Ardhi la kukatatua mgogoro nje ya Mahakama.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga na Kaimu Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Wilson Charles wakikata utepe kuashiria kusainiwa kwa mkataba wa mpango wa utekelezeji wa matumizi ya Shamba la Bwawani na Shambarai Burka liloko Wilaya ya Arusha na Arumeru Mkoani Arusha.

Aidha Eng. Sanga aliongeza kuwa baada ya serikali kulipa fidia kama ilivyokubaliana na mmiliki wa awali serikali iliweka utekelezaji wa mpango wa uendelezaji na usimamizi wa shamba hilo ambapo eneo la ekari 3,076.5 lilitengwa kwa ajili ya zaao la Mkonge.

Aidha Kiongozi huyo wa Wizara ya Ardhi aliwaambia mashuhuda wa utiaji sahihi makubaliano hayo kuwa eneo la ekari 1,355 zimetengwa kama ardhi ya akiba na ekari 1,745 zilitengwa kwa ajili wananchi na mpango kina wa matumizi anwai ikiwemo ekari 673 zenye mashamba 513 yenye ukubwa wa ekari moja moja shambarai Burka Wilayani Meru.

Naye Naibu Katibu Mkuu OR- Tamisemi Wilson Charles ameitaka Bodi ya Mkonge Nchini pamoja na uendelezaji wa Shamba hilo hususani eneo nla Bwani kuangalia namna bora ya kuwezesha na kuinua hali ya Wananchi akiwataja vijana kuwa walengwa muhimu katika ukuaji na uendelezaji uchumi katika Taifa.

Wakati huohuo Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Ndugu Missaile Musa aliwataka watendaji wa Halmashauri zote mbili kuhakikisha wanatenda haki wakati wa ugawaji maweneo ya makazi na mashamba ili kuepuka manunguniko na migogoro kati ya Wanan na Serkali.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Mwalimu Zainabu Makwinya akisaini mkataba wa mpango wa utekelezeji wa matumizi ya Shamba la Bwawani na Shambarai Burka liloko Wilaya ya Arusha na Arumeru Mkoani Arusha.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Bw. Ojugu Salekwa katika mchango wake juuu ya matumizi ya shamba hilo ameiomba Wizara ya Ardhi kuweka mpango bora wa matumizi ya ardhi iliyotengwa kama ardhi ya akiba ili wananchi wasivamie maeneo hayo na kuepusha usumbufu kwa wanasiasa na watendaji wa Mkoa wa Arusha.

Shamba hilo ambalo awali lilimilikiwa na Kampuni ya Tanzania Plantation lilikabidhiwa rasmi kwa Serikali tarehe 29, Aprili 2022 baada ya serikali na kampuni hiyo kukamilisha taratibu za kisheria na baadae serikali kulipangia matumizi kwa ajili ya wananchi na sehemu ya shamba hilo kubaki kama ardhi ya akiba.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga na Kaimu Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Wilson Charles wakisaini mkataba wa mpango wa utekelezeji wa matumizi ya Shamba la Bwawani na Shambarai Burka liloko Wilaya ya Arusha na Arumeru Mkoani Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga akiongea na baadhi ya wajumbe waliofika katika hafla fupi ya kusainiwa kwa mkataba wa mpango wa utekelezeji wa matumizi ya Shamba la Bwawani na Shambarai Burka liloko Wilaya ya Arusha na Arumeru Mkoani Arusha.