Sheria mpya ya kulinda faragha ya mtu Ulaya imeanza kutekelezwa leo Ijumaa, ikisimamia zama zinazo kusudia kulinda faragha ya raia na kurekebisha jinsi makampuni yanavyo kusanya, kutumia na kuhifadhi taarifa zao.

Sheria hiyo mpya inaanza kutumika wakati ambapo kampuni kubwa ya mitandao ya jamii Facebook ikiwa inakosolewa nchini Marekani kwa kashfa ya kushindwa kulinda faragha za watu.

Sheria ya Kulinda Taarifa Kwa Jumla ya Umoja wa Ulaya (GDPR), ambayo inakuwa iko juu ya sheria mbalimbali za nchi moja moja zilizokuwepo tangu mwaka 1995, na inazitekeleza sheria hizi kwa nguvu zaidi.

Makampuni yataendelea kukusanya na kuchambua taarifa zinazopatikana katika simu, programu za simu na tovuti mbalimbali.

Tofauti kubwa iliopo hivi sasa ni kuwa makampuni lazima yatoe sababu za kuridhisha kwa hatua yoyote inayochukuwa kukusanya au kutumia taarifa hizo binafsi.

Pia wanakatazwa chini ya sheria hii mpya kutumia taarifa hizo kwa sababu nyingine baada ya muda kupita.

Sheria hizo mpya zinatumika katika nchi 28 za Umoja wa Ulaya lakini pia zitaathiri biashara zote kubwa na ndogo nchini Marekani.

Sheria hizo zinataka makampuni kueleza wazi jinsi wanavyokusanya na kutumia taarifa hizo. Matokeo yake, kampuni zinaondoa misamiati wakati wakizifanyia marekebisho sera zinazosimamia faragha za watu.

By Jamhuri