Mkuu wa Wilaya ya Ukelewe Hassan Bomboko akiapa
Mkuu wa Wilaya ya Magu Rachel Kasanda akiapa

Wakuu wa Wilaya ya Magu na Ukerewe wameapishwa leo kufuatia uteuzi uliofaywa na Rais wa Jamuhri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani Januari 25,2023.

Uapisho huo umefanyika leo Feburuari 3,2023 kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha Wakuu hao Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela, amewataka kushirikiana na viongozi wengine katika kusimamia vizuri masula ya utawala bora kwenye maeneo yao kwa kuzingatia namna ya uendeshaji wa taratibu za nchi kwa mujibu wa sheria.

“Nendeni mkatekeleze majukumu yenu kwa kufuata Sheria,Kanuni na taratibu za nchi ili mkawatumikie vyema wananchi na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Wilaya zenu”, amesema Shigela.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza Dkt.Ntemi Kilekamajenga, amewaomba wakuu hao kuwasaidia katika utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi hata kabla haijafika mahakamani.

Amesema kwa upande wa Mahakama wanaendelea kujitahidi kusuluhisha migogoro hiyo na pale inaposhindikana wanatumia sheria japo usuluhishi unasaidia kupunguza mlolongo mrefu wa kukaa Mahakamani.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ukelewe Hassan Bomboko, amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amemkopesha Imani hivyo ana budi kwenda kuilipa kwa kuchapa kazi katika Wilaya hiyo.

“Naahidi nitakuwa mchapakazi kwani adhima yangu ni kuwa muadilifu na muanifu,pia nitasimamia haki na usawa katika Wilaya yangu sanjari na kutoa ushirikiano kwa viongozi wenzangu,falsafa yangu ni uongozi shirikishi ili kuweza kutatua kero, changamoto za wananchi”, amesema Bomboko.

Rachel Kasanda ni Mkuu wa Wilaya ya Magu amesema atahakikisha huduma zinawafikia wananchi wa Wilaya ya Magu kama zilivyokusudiwa huku adhima yake ni kusimamia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

By Jamhuri