Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi nchini limesema tarehe 22 novemba mwaka Mwaka huu litateketeza silaha haramu zilizosalimishwa kwa hiari katika kampeni maalumu iliyofanyika nchi nzima kuanzia septemba 01 mwaka hadi October 31 mwaka huu iliyokuwa ikiongozwa na kauli mbiu isemayo Silaha haramu sasa basi, salimisha kwa hiari.

Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP DAVID MISIME

Taarifa hiyo imetolewa leo novemba 20 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP DAVID MISIME ambapo amebainisha kuwa zoezi hilo litafanyika kuanzia muda wa saa 02:00 asubuhi katika Viwanja vya shabaha vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vilivyopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

Zinazohusiana

  -Polisi Shinyanga wakamata silaha zinazotumika kuendesha uhalifu

-‘Tumieni vema msamaha kusalimishasilaha mnazomiliki kinyume cha sheria’

Aidha amebainisha kuwa Mgeni rasmi katika zoezi hilo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (Mb).

SACP Misime amesemaa kuwa Jeshi hilo linawaalika wananchi Pamoja na Viongozi wa Serikali za mitaa hususani wanaoishi maeneo ya Kunduchi kuhudhuria ili kujionea mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na kampeni hiyo ya usalimishaji silaha.

By Jamhuri