Klabu ya Simba imepata ushindi wa bao 1-0 Wydad Casablanca.

Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali.

Bao la kuongoza limefungwa na mshambuliaji Jean Baleke akiwa ndani ya 18 dakika ya 30.

Dakika 45 za mwanzo Simba imepata umiliki wa asilimia 55 huku Wydad wakiwa na umiliki wa asilimia 45.

Ushindani ni mkubwa huku Wydad wao wakicheza kwa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza.

Licha ya kuwa na mabadiliko katika kikosi cha kwanza akianza Ally Salim langoni bado walikuwa na kushinda mchezo huo.

Baleke alikwama kukamilisha dakika 90 na nafasi yake ilichukuliwa na nahodha John Bocco kwenye mchezo huo.

By Jamhuri