Na Wilson Malima,JamhuriMedia,Dar

Timu ya soka ya Wanawake Simba Queens imefanikiwa kusaini mkataba wa thamani ya Sh. bilioni 01 kwa kipindi cha miaka mitano kutoka kwa kampuni ya michezo ya kubashiri M-Bet, ambapo timu hiyo itakuwa ikipokea milioni 200 kila mwaka.

Akizungumza na a waandishi wa habari Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez amesema kuwa thamani ya timu hiyo imepanda na hivyo lazima kupata mdhamini wake mwenyewe bila kutegemea kutoka kikosi cha Simba ya wanaume.

“Juzi tumeona wachezaji sita wa Simba Queen wapo kwenye kikosi cha FIFA World Cup U17, leo alfajiri wachezaji wote kwa ujumla pamoja na waalimu wameenda Morocco kwaajili ya michuano ya kimataifa

“Thamani ya Simba Queen inaendelea kupanda na tuliamua kusaini mkataba rasmi leo Oktoba 26,2022, kwa miaka mitano kwa milioni 200 kwa mwaka, Bilioni moja ndani ya miaka mitano na kila mwaka inaongeza kwa asilimia 10,” amesema.

Barbara aliongeza kuwa watawekeza pia kutusaidia na vifaa, kama unavyojua kwa sasa ligi ya wanawake haitangazwi rasmi.

Mechi zote za Simba Queen ambazo hazioneshwi kwenye mitandao zitaoneshwa kwenye Simba App kwa fursa na uwezo wa M-bet, tukianza mechi yetu ya kwanza Jumamosi Morocco wasichana wetu watavaa jezi.

Kikosi cha klabu hiyo kimefanikiwa kuwa timu pekee ya wanawake ya Afrika Mashariki kushiriki michuano ya ligi ya Afrika kwa upande wa wanawake ambapo kikosi hicho kimesafiri alfajiri ya leo kuelekea nchini Morroco kwa ajili ya michuano hiyo.