Na Tatu Saad, Jamhuri Medi.

Uongozi wa klabu ya Simba Sc umefikia makubaliano ya kumuuza nahodha wa timu hiyo kwa upande wa wanawake ‘Simba Queens’, Opah Clement kwenda kuitumikia Besiktas,nchini Uturuki

Mchezaji huyo ameshaondoka nchini tayari na kutimkia Uturuki kwajili ya kujiunga na timu yake mpya ya nchini humo.

Opah ana jumla ya mabao 9 katika ligi kuu ya wanawke ya Tanzania, akiwa ndio kinara wa magoli wa timu hiyo na ligi kwa ujumla.

By Jamhuri