Na Tatu Saad, JAMHURI

Baada ya ushindi wa bao 1-0 walioupata jana Simba Sc dhidi ya Vipers ya Uganda, Afisa habari wa klabu ya Simba Sc Ahmed Ally amesema maneno yanayozungumzwa mtaani ni kama Simba Ndio imefungwa jana.

Ahmed amefunguka katika kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa amekuwa akipokea taarifa za kukosolewa kwa kikosi chao baada ya mchezo wa jana.

“Ukisikiliza Radio unaweza kujua Simba ndo imefungwa jana, halafu ukisiliza tena unaweza kudhani Simba ndo ina point moja kwenye kundi letu, halafu ukitega sikio vizuri unaweza kuhisi kwamba Simba hakuna kitu kizuri tumefanya jana”.Alisema Ahmed.

Hata hivyo Ahmed amesema wanachotaka wao waendelee kukosolewa ili wazidi kujirekebisha ili wafike hatua ya nusu fainali.

“Ila sisi ndo tunapenda mtukosoe hadi tufike Nusu Fainali tuliyokusudia.” Ameandika Ahmed.

Ushindi wao wa jana Simba Sc umewapa nafasi ya kupanda kutoka nafasi ya pili waliyokuwa awali na kushika nafasi ya kwanza wakiwa na alama sita wakiongozwa na Raja Casablanca mwenye alama 12.

By Jamhuri