Na Magreth Kinabo –Mahakama

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema kwamba Bunge liko tayari kubadili sheria zinazoleta changamoto katika mashauri yanayohusu ukatili wa kijinsia hususan kwa wanawake ,watoto na watu wenyeulemavu.

Akizungumza jana katika mkutano wa siku mbili wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambapo alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan unaofanyika kwenye hoteli ya New Tanga Beach Resort alikishauri chama hicho kuangalia namna ya kutoa haki kwa makaundi hayo.

“Utakuta mtoto amefanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia na mtuhumiwa amekamatwa baada ya sisikujiridhisha, halafu anaachiwa sasa tunajiuliza kama mtuhumiwa ameachiwa nani ametenda kitendo hicho na mtoto na ameathirika, lakini hatuambiwi nani ametenda kosa hilo. Kama sheria zinazotumika ni changamoto sisi tuko tayari kubadilisha, ili haki iweze kutendeka,” amesema Spika Tulia.

Aliongeza kwamba kuwa ni lazima jamii ikapewa elimu kuhusu uendeshaji wa mashauri yanayohusu makundi hayo ili iwe salama nayi pia muwe salama na kila mtu awe na amani katika uendeshaji wa mashauri hayo.

Spika Tulia amesema kuwa wanachama wa TAWJA wanapotaoa hukumu anu maamuzi ya ukatili wa kijinsia watoe haki inayozingatia usawa na wakati ili mtu asione kuwa ametendewa haki kwa kutokana umasikini , mwanamke, mtoto au ni mtu mwenye ulemavu.

“Mafanikio yenu hayapimwi kwa kuzingatia hukumu au maamuzi yaliyoandikwa, idadi ya vikao vya maamuzi na idadi ya mizozo, bali yanapimwa kwa namna gani tafsiri ya hukumu au maamuzi hayo yanatoa nafasi kwa jamii kuweza kuondokana na ubaguzi na ukatili wa kijinsia,“hivyo ni wakati wa wao kusimama imara na kutekeleza majukumu yao ,”alisisitiza.

Aidha Spika huyo alisema kuwa wanachama 20 waliopatiwa mafunzo kuhusu suala hilo la namna ya kuendesha mashauri ya ukatili wa kijinsia wayatumie, kuboresha utendaji kazi, huku akisisitiza kwamba ni vizuri wanachama wanaopatiwa mafunzo wangalie kuwa mtu ana mchango gani au anatetea nini.

Amewataka wanachama hao, kutumia wakati huo muhimu kwenye mkutano huo kujadili kuhusu Mpango Mkakati wa mwaka 2023 na kuchagua viongozi wenye sifa ya kukipeleka mbele chama hicho na kutekeleza malengo yake.

Amewaasa kuendelea kuwa na maadili mema ili kuweza kuendelea kujenga heshima na kujenga imani kwa wananchi.

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Prof Ibrahim Hamis Juma alisema ni lazima uongozi wa TAWJA uweke utaratibu wa kuweka kumbukumbu na kutangaza mafanikio yanayotokana na kazi mbalimbali zinazofanywa na wanachama, ikiwemo michango mingi ya kujitolea ambayo wanachama wameitoa.

Jaji Mkuu huyo alitoa takwimu za mhimili huo za Desemba 31,mwaka jana ambazo zinaonyesha uwepo wa wanachama wa TAWJA kila kona ya Mahakama,akianzia idadi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani kuwa ni 26 ambapo kati ya hao wanaume ni 16 sawa na asilimia 62 na wanawake ni 10 sawa na asilimia 62. Idadi ya Mahakama Kuu ni 97, Majaji wanaume ni 62 sawa na asilimia 64 na wanawake ni 35 sawa na asilimia 36.

Ameongeza kuwa idadi ya Majaji Wafawidhi ni 24, wanaume ni 16 sawa na asilimia 67 na wanawake ni nane sawa na asilimia 33. Wasajili ni watatu, wanaume ni wawili sawa na asilimia 67 na wanawake ni mmoja sawa na asilimia 33, Naibu Wasajili ni 53, wanaume ni 33 sawa na asilimia 62, wanawake ni 20 sawa na asilimia 38. Idadi Ya Mahakimu Wakazi Mahakama za Mahakama za Hakimu Mkazi ni 69, wanaume ni 38 sawa na asilimia 55 na wanawake ni 31 sawa na asimilia 45.

Idadi ya Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi ni 28. Idadi ya Mahakimu Wakazi wa Mahakama za Wilaya ni 284 ,wanaume ni 141 sawa na asilimia 50 na wanawake ni 143 sawa na asilimia 59. Idadi ya Mahakimu wakazi wa Mahakama za Wilaya ni 135, wanaume ni 76 sawa na asilimia 56 na wanawake ni 59 sawa na asilimia 44. Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo ni 875, wanaume ni 408 sawa na asilimia 47 na wanawake ni 467 sawa na asilimia 53, wengine Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama za Mwanzo ni 577, wanaume ni 329 na wanawake ni 248.

“Ni muhimu zaidi kwa kila mwanachama atatumiaje uwepo wake kwa uchache wenu katika kutatua usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake ili nao wafaidiMaendeleo Endelevu na wafurahie Haki za Binadamu,”amesisitiza Jaji Mkuu huku akiwashauri kuendelea kujifunz na kufanya tafiti.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Khamis Ramadhani Abdalla,ambaye amesema ataendele kuwa na ushirikiano na chama hicho na kuongeza kwamba Zanzibar ina Majaji 12 kati yao wanne ni wanawake na Mahakimu 64 , ambapo wanawake ni 23.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Omary Mgumba aliomba vyombo vya usafiri vinavyokamatwa katika biashara haramu vishikiliwa, akiwemo mtuhumiwa hadi kesi itakapoisha.

Naye Mwenyekiti ws Chama cha TAWJA ambaye pia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Joaquine De Mello amesema chama hicho ina wanachama 300.

By Jamhuri