Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati)   alipojumuika na Waumini mbalimbli na Viongozi  katika ibada ya swala ya Ijumaa leo  katika Masjid Al- Rahmah Mombasa,Mkoa wa Mjini Magharibi .[Picha na Ikulu] 01/09/2023 .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)  alipokuwa akitoa nasana zake kwa Waumini mbalimbli na Viongozi mara baada ya kumalizika kwa  ibada ya swala ya Ijumaa leo  katika Masjid Al- Rahmah Mombasa,Mkoa wa Mjini Magharibi .[Picha na Ikulu] 01/09/2023 .
Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria Ibada ya Swala ya Ijumaa leo, Masjid Al- Rahmah Mombasa,Mkoa wa Mjini Magharibi wakiitikia Dua Iliyoombwa baada ya  ibada hiyi iliyojumuisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi na Viongozi mbali mbali. [Picha na Ikulu] 01/09/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)  alipokuwa akisalimiana na Khatibu wa Swala ya Ijumaa Masjid Al- Rahmah Sheikh Mussa Ali Mohamed leo mara baada ya kumalizika kwa  ibada hiyo.[Picha na Ikulu] 01/09/2023 .

………………………………………………………………………………………………………….

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewaomba waumini wa dini ya Kiislam nchini kuendelea kumuombea dua njema na kuliombea taifa kuendelea na amani, utulivu mshikamano na ushirikiano wa watu wake kwa nia ya kuendeleza maendeleo yaliopo.

Al hajj Dk. Mwinyi aliyasema hayo Msikiti wa Ijumaa Masjid Al Rahman Mbombasa Wilaya ya magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi alipojumuika pamoja na waumini wa dini ya Kiislam kwenye ibada ya sala ya Ijumaa.

Dk. Mwinyi aliwaomba waumini hao wasichoke kumuombea du’a kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwaombea viongozi wengine wa Taifa kwani wanamajukumu makubwa ya nchi kuyatekeleza na kuyafanikisha.

“Tunaomba dua zenu kwasababu tunazihitaji, majukumu tuliyonayo yakuongoza makubwa na mazito, yanahitaji du’a, kila tunapokutana kama hivi tunaomba mtuombee du’a Mwenyezi Mungu atupe wepesi kwenye majukumu yetu” alisisitiza Al hajj Dk. Mwinyi.

Pia Al hajj Dk. Mwinyi aliwashukuru waumini hao na kueleza kufurahishwa kwake kwa kujumika nao pamoja kwenye ibada ya sala hiyo.

Mapema akizungumza kwenye ibada hiyo, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume aliwahimiza waumini wa Masjid Al Rahman na wengine kwa ujumla kujiwekea utamaduni wa kukinai na kuridhika kwa neema walizojaaliwa na Allah (S.W).

Nae Khatibu wa ibada ya sala ya Ijumaa msikitini hapo, Shekh Mussa Ali Mohammed wakati akihutubu, aliwausia waumini wa dini ya Kiislam kuongeza jitihada kwenye ibada zao ili kufuzu mitihani ya Mwenyezi Mungu sambamba na kuangalia fasi zao kwa kujikinga na tamaa za matamanio ya nafsi kwa kutenda mema na kujiepusha na maovu aliyoyachukia Mwenyezi Mungu (S.W).

Wakati huo huo, Al Hajj Dk. Mwinyi aliwajuulia hali baadhi ya wazee wa jimbo la Kwahani akiwemo Mzee Nassir Ali Kombo na Said Alawiy pamoja na kuitembelea familia ya Marehemu Bi Khadija Abbas Rashid, Kwenda kutoa mkono wa pole kufuatia kifo chake kilichotokea hivi karibuni.

Marehemu Bi Khadija Abbas alikua ni mmoja wa walioshiriki zoezi la kuchanganya udongo wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar kwenye sherehe za kutimiza mwaka mmoja wa maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanzania mwaka 1965.

By Jamhuri