Na Magrethy Katengu, Jamhuriamedia, Dar es Salaam

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara,Kilimo na Mifugo imelipongeza Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kwa jitihada wanazozifanya za ukarabti wa miundombinu ili kusaidia kuinua uchumi wa bluu kupitia sekta ya uvuvi.

Pongezi hizo zimetolewa Machi,18,2024 Jijini Dar es Salaaam na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Deo Mwasanyika walipotembelea Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kukagua Mradi wa ikarabati wa miundombinu ya shirika hilo ikiwemo ujenzi wa ghala la kuzalisha Barafu ,kiwanda cha kutengenezea vyakula vya Samaki na ,ujenzi soko la samaki la kimataifa.

“Sisi Kamati ya Bunge tunawapongeza sanaa kwa kusimamia Maono ya Rais maana kila tulipopita tunakutana matokeo ya kufufua mashirika yaliyoshindikana na hapa tumebaini namna mnavyofanya kazi kwa jitihada kubwa na mmetueleza tayari mradi wa kuzalisha barafu umeanza kufanya kazi hongereni sanaa huku mkishughulikia ununuzi wa Meli nne na kuangalia ujenzi wa soko la kimtaifa la samaki ” amesema.

Hata hivyo amewasisitiza kuhakikisha wanakamilisha miradi waliyopewa kwa wakati na kusimamia fedha zilizotengwa ziefanye kazi iliyokusudiwa na kutatua changamoto ya soko la samaki iliyokuwa inalalamikiwa muda mrefu na wavuvi .

Awali akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kwa kamati hiyo Afisa Mkurugenzi Mtendaji TAFICO Dennis Simba amesema wizara ya Mifugo na Uvuvi itahakikisha miradi iliyo chini ya Program ya AFDP ya ununuzi wa meli nne za Uvuvi wa Bahari kuu, Ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mazao ya uvuvi , ujenzi wa kiwanda cha kutengengeneza chakula cha samaki, ununuzi wa samani za ofisini na kompyuta pia ununuzi wa magari ya ofisi manne ya kusimamia mradi kutekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka mfuko wa Kimataifa wa kuendeleza kilimo (agriculture)

“Uwekezaji huu ni wa muhimu sana unakwenda kunufaisha nchi kupitia raslimali za uvuvi zilizopo katika ukanda wa Uchumi bahari Miliki kwani kwa muda mrefu Taifa limekuwa halinufaiki kikamilifu na raslimali hizo hususani zilizoko baharini na hivyo sasa tunakwenda kuleta mapinduzi ya uchumi wa bluu ” amesema Afisa Mkurugenzi Mkuu

Aidha Serikali kupitia Shirika la Uvuvi TAFICO itasaidia kuongezaka ajira na Mapato ya fedha za ndani na za kigeni kusaidia kukuza pato la Taifa pia kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza zaidi katika uvuvi,ukuzaji viumbe maji,uchakataji,pamoja na mauzo ya mazao ya uvuvi hapa nchini kwa kutumia mbinu na teknolojia ya kisasa.

By Jamhuri