Katika hali isiyotarajiwa Spika wa Bunge Tulia Ackson ameharisha kwa muda kikao chake wakati wabunge wakiendekea kwenye kipindi cha maswali na majibu leo Juni 27, 2023 baada ya king’ora kinachoashiria kuna jambo la hatari.

“Waheshimiwa wabunge hiyo sauti inaashiria tutoke humu ndani kwa kwa haraka sana, kila mmoja atafute mlango wa kutoka na sote twendeni lile eneo la kukusanyikia, naahirisha shughuli za Bunge hadi hali itakapotulia’ amesema.

By Jamhuri