Na Robert Okanda,JamhuriMedia

Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, chupa za maji 5,000 zilizotumika zikiwa zilipambwa vizuri, kwa kunakshiwa kama urembo kwenye nguzo za minara ya Kirumi zinazosalimia mtu anapoingia kwenye Klabu ya Afya ya Colosseum Masaki mjini Dar es Salaam.

Ubunifu huo wa kisanaa ulifanywa na Shafina Jaffer kwa lengo la kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, kwa sasa umebadilishwa na kuwa katika mwonekano mpya wa kisanaa kazi iliyofanywa na msanii huyo wa Kitanzania na kupewa kichwa kisemacho: Tunazama.

Kwa sasa Shafina Jafer anafanya shahada ya uzamili ya uchoraji katika Chuo cha Sanaa cha Royal kilichopo London nchini Uingereza na amekusanya watu wengi kwenye bwawa la kuogelea la mita 25 katika ukumbi wa michezo ya viungo wa Colosseum akiwa na chupa za plastiki kama zile za mwanzo katika maonesho ya awali.

Kitu cha tofauti ni kwamba safari hii amezitengeneza kwenye umbo la duara au pete huku kila chupa ikiwa na rangi tofauti ya upinde wa mvua kuadhimisha Siku ya Amani Duniani.

Leo hakuna raia wa dunia hii anaweza kuchukulia kwa mzaha mabadiliko ya tabianchi tunayopitia kuanzia tufani au vimbunga nchini Marekani hadi mafuriko ya kibiblia nchini Pakistan ambapo hakuna mwanamilia wa dunia hii hajaathirika kutokana na athari za kibinadamu kwenye mazingira.

Hivyo sanaa hiyo ya kisasa ya Shafina inatoa ujumbe mzito kwa jamii ya watu wa Dar es Salaam kwa kuongeza uelewa kuhusu suala la uchafuzi wa mazingira unaowakabili watu wote.

Akiwa mbele ya vyombo vya habari vya magazeti ya Tanzania na mbele ya watoto zaidi ya 200 wa Shule ya Aga Khan ya Dar es Salaam, Shafina aliingia kwenye maji na kuogelea kwenye kipande chake cha maonesho.

Alianza kuogelea katikati ya chupa hizo za plastiki, Shafina alitaka kuonesha namna ilivyo vigumu kwa maisha ya viumbe baharini kuishi kwenye maji kutokana na tabaka za takataka za plastiki huku wakipumua kwa shida.

Aidha, katika uchambuzi wa kina wa maonesho ya Shafina, mtu anaweza kuona namba ambavyo chupa za zinavyoelea na kuchangia kujaza uchafuzi baharini na kuhatarisha maisha ya viumbe baharibi.

Jambo ambalo linamsumbua na kumvunja moyo zaidi ni namna ya kupata njia ya kuondokana na janga hilo ambalo pia Tanzania imeathiriwa.

“Tunachangia katika tatizo hilo kutokana na mazaoe yetu ya matumizi ya plastiki na kuhatarisha maisha ya viumbe bahari,” anasema.

Ili kuainisha kiwango cha uharibifu,Kisiwa cha takataka kinachopatikana kati ya California na Hawaii kinachojulikana kama ‘Great Pacific Garbage Patch’ ambacho ni mara tatu ya ukubwa wa Ufaransa na ndio hifadhi kubwa zaidi ya taka za baharini duniani kikiwa na vipande Bilioni 1.8 vya plastiki zinazoelea ambazo huua maelfu ya viumbe baharini kila mwaka.

“Tunaweza kurekebisha tabia zetu kwa urahisi huku tukitengeneza matokeo chanya kwa kubadilika kutokana na matumizi ya plastiki kwa kutumia na kuijaza tena au kwa kutotumia vitu vya plastiki,” anasema.

Sanaa ya Shafina ni ukumbusho kwa watazamaji kwamba wanapaswa kuwa makini na mazingira na kuishi maisha ya ufahamu siyo tu kwa kizazi chetu bali pia kwa kizazi kijacho.

Shafina anaendelea na safari yake ya sanaa na athari nchini Tanzania huku akifanyia kazi mradi wake ujao ambapo analenga kutumia aina mbalimbali za takataka ili kuleta tahadhari kuhusu uharibifu wa jiji na dunia kwa kutumia na utupaji wa takataka usio sahihi ambazo zinaharibu mzunguko wa maisha.

By Jamhuri