Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia,Dar es Salaam

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kinondoni imesema katika kipindi cha miezi mitatu Januari hadi Machi ,2024 wamefanikiwa kupokea jumla ya malalamiko 84 ambapo yaliyohusu rushwa ni 40 yasiyohusu rushwa ni 44.

Amebainisha hayo leo jijini Dar es Salaam Apri 23 ,2024 Naibu Mkuu Takukuru (M) Kinondoni Elizabeth Mokiwa amesema kuwa malalamiko ambayo hayakuhusu rushwa walalamikaji wengine wameshauriwa na mjadala kufungwa huku wengine wameelekezwa sehemu sahihi ya kupeleka malalamiko yao yanayohusu rushwa majalada yanaendelea kushughulikiwa katika hatua mbalimbali.

” Mchanganuo malalamiko tuliyoletewa asasi binafsi 35 ,TAMISEMI/ Manispaa19, Mahakama 6 Polisi 7, Benki 5, Elimu 3, Wizara ya Ardhi 2, TLB 1,Dini 1, JKT 1, NIDA 1, TRA 2, DAWASA 1 pia katika kipindi husika mashauri mawili 2 yametolewa maamuzi na Jamuhuri imeshinda na tumefungua mashauri mapya matatu 3 huku mashauri 19 yanaendelea mahakamani “amesema Elizabeth.

Sambamba na hayo TAKUKURU Kinondoni inaendelea kufuatia miradi 6 yenye thamani ya shilingi Bilion sitini na moja mia tisa na kumi laki saba na arobaini na sita elfu a miambili themanini na nne (61,910,746,284,.42) na wamebaini mapungufu machache ambayo wahusika wameshauriwa kurekebisha hayo na wanaendelea kufuatia hadi miradi itakapokamilika.

“Tutaendelea kutoa elimu ya rushwa na dawa za kulevya kwa vijana walioko mashuleni kupitia Vipindi vya Tv redio na Magazeti pia warsha mbambali ili watambue madhara ya rushwa na dawa za kulevya na kuchukua hafua kwa maslahi ya Taifa”amesema

Aidha wananchi wa Kinondoni wamepewa wito kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU na wanapopata taarifa zozote za rushwa watoe taarifa kuputia kupia au ujumbe mfupi namba ya dharura 113 ni bure

By Jamhuri