Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwaonesha waandishi wa habari kifaa maalumu kinachojulikana kwa jina la DOZEE ambacho kinawekwa chini ya godoro la mgonjwa akiwa nyumbani na kuweza kusoma shinikizo la damu, kiwango cha hewa mwilini, mapigo ya moyo na umeme wa moyo iwapo kutakuwa na shida taarifa itatumwa moja kwa moja kwa daktari kupitia simu yake ya yake ya mkononi ambayo imeunganishwa na kifaa hicho.

…………………………….

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeanzisha huduma ya kuwahudumia wagonjwa wakiwa majumbani (home based care) ambayo itasaidia kupunguza gharama ambazo mgonjwa uzitumia akiwa hospitalini.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitagaza huduma hiyo leo Aprili 23, 2024 Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Piter Kisenge amesema kupitia huduma hii mpya wagonjwa wa moyo watatembelewa na madaktari wakiwa nyumbani .

Dkt Kisenge amesema kupitia huduma hiyo watapewa kifaa kinachoitwa Dozee ambacho kitawekwa chini ya shuka katika kitanda cha mgonjwa.

Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwaonesha waandishi wa habari kifaa maalumu kijulikanacho kwa jina la DOZEE kinachotumika kufuatilia maendeleo ya mgonjwa anayetibiwa akiwa nyumbani huku daktari akipata taarifa zote kupitia simu yake ya mkononi ambayo imeunganishwa na kifaa hicho.

“Kupitia huduma hii wagonjwa wa moyo wanaohitaji mwendelezo wa matibabu kwa sasa hawatakuwa na haja kufika hospitali kila wakati badala yake watapatiwa huduma hiyo wakiwa nyumbani “amesema Dkt Kisenge

Aidha amesema kifaa hicho kitakuwa kikipima mapigo ya moyo , Oksijeni ya mgonjwa, shinikizo la damu pamoja na kutoa taarifa kwa madaktari.

Aliendelea kueleza kuwa huduma hiyo itasaidia kupunguza vifo vya gafla ambavyo vimekuwa vikiwakumba wagonjwa.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Moyo Dkt Smita Bhalia amesema huduma hiyo pia itatoa elimu ya lishe ,huduma ya Magari ya dharura(Ambulance) pamoja na matibabu ya dawa .

Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) Smita Bhalia akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam aina za huduma za kuwafuata wagonjwa majumbani mwao na kuwapatia tiba wanayostahili zinakazotolewa na Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge.
Limited Pankaj Kumar akimuonesha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge mfano wa taarifa za mgonjwa aliyeko nyumbani ambaye amefungiwa kifaa kinachojulikana kwa jina la  DOZEE zinavyoonekana kupitia simu ya mkononi ya daktari aliyeunganishwa na kifaa hicho.

By Jamhuri