Na Benny Kingson,JamhuriMedia,Tabora

Watumishi wanne wa Chuo Cha Mafunzo Stadi (VETA), mkoani Tabora wamefikishwa mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),kufuatia kufuja fedha sh.mil.750 za ujenzi wa chuo wilayani Uyui ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa alilitoa hivi karibuni akiwa ziarani mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa TAKUKURU mkoani Tabora Musa Chaulo, akati akitoa taarifa ya utekelezaji kazi kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2022 amesema kuwa watumishi hao wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ubadhilifu huo.

da cha mlinzi katika  Chuo cha VETA  Uyui mkoani Tabora ambacho kimejengwa kwa gharama ya sh.milioni 11. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikagua ujenzi wa Chuo hicho, Septemba 8, 2022 aliagiza TAKUKURU iwakamate waliosimamia  ujenzi huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Chaulo amesema kuwa kwa kuwa kesi hiyo tayari ipo mahakamani hana mamlaka ya kuiongelea na kutaja majina ya wahusika hadi pale mahakama itakapotoa maamuzi dhidi ya wahusika na kwamba wametekeleza agizo la Waziri Mkuu alilolitoa akiwa ziarani mkoani hapa hivi karibuni.

“Mtakumbuka Wazri Mkuu aliagiza tuwakamate wale wote waliohusika kuhujumu pesa za Serikali katika kutekeleza ujenzi wa chuo cha VETA qilayani Uyui,alistukia ubadhilifu huo kwa kibanda cha mlinzi kutumia zaidi ya sh.m.11 na majengo mengine ya nyumba za wakufunzi kugharimu pesa nyingi kinyume na uhalisia”amesema.

Kamanda huyo amesema kuwa wamefuatilia na kukagua jumla ya miradi 14 ya maendeleo katika sekta za elimu.afya,maji na ujenzi yenye thamani y a sh.b.11,326,856,108.9 ikiwa ni pamoja na ukarabati wa viwanja vya michezo katika shule ya sekondari wavulana na wasichana za Tabora.

Amesema kuwa katika ukarabati wa viwanja hivyo wakati wa maandalizi ya michezo ya umoja wa shule za msingi Umitashimta na yale ya shule za sekondari Umiseta ambapo wanafuatilia ubadhilifu ulifanyika ikiwa ni pamoja na gharama halisi zilizotumika kuendesha michezo hiyo ambayo kitaifa ilifanyika mkoani hapa mwaka huu.

Kwa upande wa fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 zilizotolewa na Serikali kwa Mkoa wa Tabora katika halmashauri na idara zinazosimamiwa na serikali kuu kama TANAPA,TAWA,VETA,MAMLAKA ZA MAJI NA MAWASILIANO ambapo jumla ya sh.4,470,750,000.00 wamezifuatilia.

Chaulo ametaja miradi waliyoifuatilia kuwa ni pamoja na ujenzi wa CHUO CH veta Wilayani Uyui sh.750,000,000.00 na kesi 1 imefunguliwa na uchunguzi unaendelea,ujenzi wa vymba vya madarasa 34 katika shule za msingi na sekondari wilayani Kaliua sh.3,700,000,300.00 hapakuwa na ushindanishi wakati wa kununua vifaa vya ujenzi kwa baadhi Ya shle n uchunguzi unaendelea.

Ametaja miradi mingine ni ununuzi wa vifaa vya kujikinga na UVIKO 19 katika Manispaa ya Tabora,sh.17,000,000.00 na palibainika manunuzi hewa,jalada la uchunguzi limepelekwa NPS kupata kibali cha mashitaka,ununuzi wa vifaa vya kujikinga na UVIKO 19 katika halmashauri ya Wilaya ya Igunga,sh.3,750,000.00 ambapo ilibainika kuwapo kwa nyraka zilizoghushiwa katika marejesho ya fedha,uchunguzi unaendelea.

By Jamhuri