TANESCO yasitisha matengenezo ya LUKU

MATENGENEZO kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku yaliyokuwa yaanze Agosti 22 hadi 25, kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi yamesitishwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya muda mchache Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutangaza matengenezo kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku ambayo yangesababisha kukosekana kwa huduma hiyo.

Meneja Mwandamizi wa Tehama wa shirika hilo, Cliff Maregeli amesema matengenezo hayo ya siku nne yalikuwa yaanze Agosti 22 hadi 25, mwaka huu kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi sasa yamesitishwa.

Amesema kutokana na matengenezo hayo, wananchi wasingeweza kununua umeme kwa njia ya Luku.

Amesema lengo la matengenezo hayo ni kuongeza ufanisi katika mfumo wa Luku.