Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Serikali kupitia Wizara ya Wizara ya Mipango na Uwekezaji kuhakikisha wanaendelea kuweka mazingira mazuri ya kufanyabiashara na uwekezaji ili kusaidia Tanzania kukua kiuchumi.

Kuhusu uwekezaji katika eneo la Sinotan amesema wanatarajia kuona uwekezaji huo utakuwa na faida nyingi kwa Watanzania wote wakiwemo wa Kibaha mkoani Pwani.

Awali Mwenyekiti wa Bodi wa Kituo cga Uwekezaji Tanzania( TIC), Dk.Binilith Mahenge ametumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini.

Kuhusu eneo la uwekezaji uliofanywa na Sinotan Industrial Park, Dk.Mahenge amesema eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya uwekezaji ni hekta 2500 na kiasi cha fedha cha fedha ambacho kimewekezwa ni Dola za Marekani milioni 327 huku Opereta wakitarajiwa kuweka zaidi ya dola za Marekani Bilioni tatu.

Aidha amesema katika eneo hilo awali eneo hilo lilikuwa na changamoto ya kuchelewa kuwepo kwa vivutio vya uwekezaji lakini Serikali kupitia TIC wamemaliza changamoto na tayari kuna vivutio.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Group Six Internatiaonal , Sinotan Industrial Park Janson Huang amefafanua kwa kina kuhusu uwekezaji unaoendelea kufanywa eneo hilo sambamba na wawekezaji kutoka China kuonesha kiu ya kujenga viwanda katika eneo la Sinotan..