Tanzania na Oman zameweka mikakati ya ushirikiano katika sekta ya Mawasiliano, Habari na Teknolojia ambapo nchi hizi mbili zinaweza kutumia vyombo vyake vya habari kuhabarisha umma katika masuala mbalimbali ya kijamii, kutangaza tamaduni na kubadilishana ujuzi wa teknolojia.

hayo yamebainishwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati alipokutana na Waziri wa Habari wa Oman Mhe. Dkt. Abdullah bin Nasser bin Khalifa Al-Harassi tarehe 23 Novemba, 2022, nchini Oman.

Katika mazungumzo yao Waziri Nape ameeleza kuwa, kutokana na mahusiano ya kihistoria ya muda mrefu kati ya Tanzania na Oman, nchi hizi zinapaswa kuhabarishwa ipasavyo juu ya undugu wa damu kati ya watu wa Oman na watanzania ili kuendelea kutunza uhusiano huo na kukubaliana kuwa Oman kupitia vyombo vyake vya habari itaitangaza Tanzania katika mataifa mengine ili kuvutia biashara, uwekezaji na utalii.

By Jamhuri