Na Wilson Maliama, JAMHURI MEDIA

Makoa wa Rukwa umetajwa kuwa kinara wa wizi wa fedha  kwa njia ya mtandao kwenye simu unaofanywa na watu wasio waaminifu huku watumiaji wa mtandao wa Tigo ndiyo wakionekana kuibiwa kwa wingi kuliko mitandao mingine yoyote.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya robo ya mwaka ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) kwa kipindi cha Mwezi Januari hadi Machi, 2023.

“Muhtasari unaonyesha kuwa kwa asilimia kimikoa, Rukwa inaongoza kwa kuwa na wizi wa fedha za simu kwa asilimia 45 ya wizi wote ulioyokea  kati ya Januari na Mchi, 2023” Inasema taarifa ya TCRA

Ripoti ya mamlaka hiyo inasema kuwa katika taarifa iliyopita Morogoro ndiyo ilikuwa kinara kwa wizi huo ingawa kwa sasa imeshuka na kushika nafsi ya pili ikiwa na silimia 18 ambapo inafuatiwa na Dar es Salaam asilimia 14, Mbeya asilimia 7, huku mikoa ya Mwanza Arusha, Dodoma, Pwani na Kagera ikichangia kwa asilimia 1.

Aidha kwa upande wa watoa huduma ripoti hiyo imeutaja mtandao wa Tigo kuongoza kutumika katika wizi uliofanyika, ambapo kati ya Vodacom Airtel na TTCL mtandao huo umeongoza kwa asilimia 34.

“Kwa upande wa mitandao ya simu inaonekana wizi uliofanyika Tigo inaongoza kwa kuwa na asilimia 34 ikifuatiwa na Airtell asilimia 32, Vodacom asilimia 28 na TTCL asilimia 3” Inasema taarifa ya TCRA

By Jamhuri