Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limefanya ziara katika ofisi tatu za Mkoa wa Lindi, kutoa shukrani kwa ushirikiano walioupata wakati wa Mkutano Mkuu wa Saba wa jukwaa hilo uliofanyika mkoani humo.

Maofisa wa jukwaa hilo walitembelea katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Katika kutambua mchango wao, Balile aliwakabidhi vyeti vya shukrani ikiwa ni kutambua ushirikiano wao katika kufanikisha mkutano huo.

Katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi, Balile alikabidhi cheti hicho kwa Afisa Maendeleo ya Jamii, Moses Mkoveke kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa hiyo Juma Mnwele ambaye alikuwa safarini, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemaga na Mkuu wa Mkoa, Zainab Telack walipokea vyeti vyao wenyewe.

Viongozi hao wameomba wafahariri kuendelea kutangaza fursa zilizomo katika mkoa huo na kwamba, milango ya uwekezaji mkubwa na mddogo ipo wazi.