Tetemeko la ardhi Uturuki,vifo vyafikia 4,800

Idadi ya vifo inaongezeka hadi sasa zaidi ya 4,800 vimerekodiwa kutokana na tetemeko lilitokea siky ya Jumatatu.

Nchini Uturuki, idadi ya watu ambao wamekufa kwa sababu ya matetemeko haya ya ardhi imeongezeka hadi 3,381, kulingana na mamlaka ya maafa nchini humo.

Orhan Tatar, afisa katika Mamlaka ya Usimamizi wa Maafa na Dharura (AFAD), anasema wengine 20,426 wamejeruhiwa na majengo 5,775 yameporomoka.

Hesabu hiyo mpya inafikisha idadi ya waliofariki nchini Uturuki na nchi jirani ya Syria kufikia 4,890. Idadi hii huenda ikazidi kuongezeka.