na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekutana na waandishi wa habari kujadili namna bora ya kuwafikishia habari wananchi juu utabiri wa mvua za msimu wa vuli unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba mpaka mwezi Desema mwaka huu.

Akizungumza wakati wa ufunguaji wa warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika jijini Dar es Salaam , Dkt. Ladislaus Chang’a Kaimu Mkurugenzi wa TMA amesema kuwa kufikisha habari sahihi za utabiri wa hali ya hewa ni nyenzo bora kuongeza ufanisi katika shughuli za uchumi na zile za kijamii.

Dkt. Chang’a amesema kuwa habari za utabiri sahihi huwewezesha wananchi kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na utabari huo.

Dkt. Chang’a ametanabaisha kuwa waandishi wa habari wamekuwa sehemu ya Mamlaka kwa kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi na kusaidia wananchi pamoja na serikali kujiandaa na majanga yaliyotokana na Hali ya hewa kama vile mvua za Al Nino na Kimbunga Hidaya.

Amesema kuwa semina na kuwa karibu na waandishi wa habari kumesaidia taarifa za tabiri kufika kwa wananchi kwa wakati na kusaidia kwenye shughuli za kiuchimi.

Semina hiyo iliyobebwa na kauli mbiu ya matumizi sahihi ya taarifa za Hali ya Hewa kwa wote na kwa wakati ilihudhuriwa na waandishi zaidi ya 27 kutoka vyombo vya habari mbalimbali nchini .

Naye Dkt. Hamza Kabelwa Mkurugenzi wa Huduma ya Utabiri TMA amesema kuwa kukutana na waandishi wa habari kutaendelea kuwasaidi wananchi na kuisaidia nchi katika kujiandaa na majanga na kujua wakati sahihi wa kufanya shughuli za kiuchumi.
Please follow and like us:
Pin Share