Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Dar

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa kwa baadhi ya maeneo ya Ziwa Nyasa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA imesema kuwa tahadhari hiyo inaanza leo huku Septemba 24 na 25, 2022 kukiwa hakuna tahadhari.

Taarifa ya TMA imesema, athari zinazoweza kujitokeza ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi na usafirishaji majini.

TMA imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa kwa baadhi ya maeneo ya Ziwa Nyasa (mikoa ya Ruvuma na Njombe).

“Hizo siku mbili hazina athari, tumeziweka kwa sababu ripoti lazima izingatie kipindi cha siku tano,” amesema Rose Tenyagwa, mtaalamu TMA

By Jamhuri