Na Benny Kingson, JamhuriMedia, Tabora
Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba kanda ya magharibi TDMA imekamata jumala ya daza za milioni 2 zikiwemo ‘vega’ na sigara dawa amazo ni hatari kwa matumizi.
Meneja wa TFDA Kanda hiyo Dk.Christopher Migoha akitoa taarifa ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai mwaka 2023 hadi Machi 2024 amabpo walkamata madawa hayo yenye thamiani y ash.milioni 3,972,017.
Dk.Migoha amesema kati ya dawa hizo walikamata sigara dawa zenye thamani y ash.milioni 2,100,011 ikiwa ni jumla ya sigara 8,642, sigara za Kongo 2,140 na klabu 1,038 kutoka nchini India na kuongeza kuwa matumizi ya madawa hayo yana madhara makubwa kwa afya kwa kuwa yanaongeza msukumo wa damu mwilini.
“Dawa hizi ni hatari kwa afya za jamii kwa kuwa yanamfanya mtumiaji awe na msukumo mkubwa wa damu mwilini,kitendo kinachoathili mfumo wa upumuaji na ubongo na kusababisha matatizo ya kisaikolojia na kufanya wakose kujiamini bila kuyatumia”alisema.
Meneja huo amesema katika kipindi hicho wame baini madawa hayo hususani sigara dawa hizo zitoka katia nchi za India,Burundi na Kongo ambapo nyingi ya sigara hizo wamezikuta zimemalizika muda wake wa matumizi lakini jamii imekuwa ikiZinunua nakuzitumia.
Amesema kuwa kama wazalishaji wa bidhaa hizo wanahitaji kuendelea kufanya biashara,wanatakiwa kufuata utaratibu wa kuweka maandishi makubwa yanayoonyesha madhara yanayokana nayo kama ilivyo kwa bidhaa nyingine ili kuweka tahadhari kwa watumiaji.
Amesema katikaukaguzi huo wamekagua mifumo ya 30 ya mionzo ‘x-ray’,m-ray na’ utra sound’ ambapo walibaini mifumo 5 haifanyikazi na 25 peke ndiyo inayofanyakazi ikiwa ni sawa na asilimia 85 ambapo pia wamefanya ukaguzi wa maduka ya madawa 18 ya jumla,39 rejareja,kubaini maduka 10 yenye mifuko isiyoruhusiwa,maduka 400 ya dawa baridi,maduka 54 ya mifugo ,hospitali 37 na vituo 48 vya afya.
Dk.Migoha amesema katika kipindi hichi wamefanikiwa kukusanya jumla y ash.milioni 10 kupitia malengo yao 6 ya kudhibiti na 4 mtambuka udhibiti na kuhakikisha ufanisi wa vitendanishi na kwamba wana hudumia katika Mikoa ya Tabora,Kigoma na Katavi.
Amesema wataendelea kuongeza nguvu zaidi katika kudhibiti,kutoa elimu na kuhakikisha watoa huduma wanafuata sherika,kanuni na miongozo pia kuwa wazalendo badala ya kujalai maslahi yao na kuhakikisha afya za jamii zinalindwa daima.
Amewata wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa TDMA kwa kuwapa taarifa za wahusika wanafanya shughuli za kutoa huduma kinyume na maagizo ambapo watachukua hatua kali dhidi ya watakaobainika bila kujali wana umaarufu ama vyeo vikubwa.